Msaada
Msaada kuhusu papershot.
Majibu mafupi kwa maswali tunayoulizwa zaidi. Kwa jambo lingine lolote, tuandikie.
Maswali ya kawaida
Ninajiungaje na tukio?
Skani kadi ya mwaliko ya mwenyeji kwa kamera ya simu yako, au fungua kiungo cha mwaliko. Unahitaji programu ya papershot kwenye iPhone au Android, lakini huhitaji akaunti.
Picha huhifadhiwa kwa muda gani?
Tukio la bure huhifadhi roli yake saa 48 baada ya kufungwa, na tukio lililolipiwa siku 30. Hifadhi unachotaka kubaki nacho kabla ya hapo.
Ninahifadhije picha kwenye simu yangu?
Fungua picha na uihifadhi kwenye maktaba yako. Ili kuhifadhi nyingi kwa mara moja, zipakue pamoja kama faili moja la .zip.
Ninaripotije kitu kwenye roli?
Kifungue, gusa Ripoti, kisha chagua sababu. Kinatoweka kwenye roli yako mara moja, na tunakikagua ndani ya saa 24.
Ninafutaje akaunti yangu?
Kwenye programu, fungua Mipangilio na uguse Futa akaunti. Matukio unayoandaa, pamoja na kila kitu kilichomo, yanaondolewa mara moja. Ulichoongeza kwenye matukio ya watu wengine kinabaki kwenye roli zao, na jina lako huondolewa akaunti yako inapofutwa kabisa baada ya siku 30.
Naweza kurejeshewa pesa?
Ununuzi hupitia Apple au Google, kwa hiyo marejesho hufuata sheria zao. Omba kupitia duka ulilonunulia.
Bado unahitaji msaada?
Tuandikie kwa support@papershot.app. Tuambie ni tukio gani na unatumia simu gani.
